DRC

Mapigano makali yameripotika kati ya jeshi la serikali na waasi wa M23 karibu na Mji wa Kanyabayonga wilayani Rutshuru na kusababisha hofu kubwa miongoni mwa wakaazi.

JUNI 19, 2024
Border
news image

Akizungumuza na MTV News DRC ,Kasereka Swing wa shirika la raia katika Mji wa Kanyabayonga wilayani Lubero asema milio ya risasi inasikika kila sehemu pembezoni mwa Mji wa Kanyabayonga ambako pande tatu za shuhudia mapigano makali tangu asubui ya leo juni kumi na tisa elfu mbali ishirini nan ne ,waasi wa M23 wakijaribu kuingia katika Mji wa Kanyabayonga bila mafanikio .

Taarifa za sasa azasema bomu toka upande wa M23 zimeanguka katika eneo la Bulotwa na kuangukia makaazi ya watu ,hadi sasa tukiwa bado hatuja pata matukio Zaidi baada ya bomu kadhaa kuangikia watu kwenye sehemu mbali mbali.

Jeshi la serikali likishirikiana na wazalendo wakitwangana vikali na M23 ambao kwa sasa inapata Msaada wa Rwanda na Uganda kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa .M23 imekuwa ikomba mazungumuzo na serikali ya Kinshasa ,na Kinshasa ikisema haiwezekani kuzungumuza na M23 kwani ni tawi la jeshi la Rwanda ndilo lina tatiza usalama wa Congo.Huku Rwanda ikisema ipo kwenye Ardhi ya DRC kulinda usalama wa wananchi wake dhidi ya wapiganaji ambao yaita FDLR.

AM/MTV News DRC