DRC

Mapigano makali yaendelea wilayani Rutshuru Kivu Kaskazini mashariki mwa Congo DRC kati ya M23 na jeshi la serikali ya FARDC

JUNI 03, 2024
Border
news image

Akizungumuza na MTV News DRC kasereka Swing kutoka shirika la raia katika mji wa kanyabayonga wilayani Lubero asema milio ya sialaha nzito imendelea kusikika katika Mji wa Kanyabayonga kutoka eneo la Mapigano ambako jeshi la Congo FARDC lapambana sasa kwa siku tanu na waasi wa M23 ambao walionekana kusonga mbele mweishoni mwa Wiki ila kwa sasa wakizuliwa na jeshi tiifu kwa serikali FARDC.

Swingi amesema kwa sasa wananchi wa Mji wa kanyabayonga waote wamekimbia kutokana na uasi wa M23 ila sehemu ndogo wakiwa wanaume ndio wapo mjini Pamoja na vijana wanao jitolea na kukataa Mji wao kuanguka katika uasi wa M23 bado wanaenedele kuonekana .sehemu kubwa wakiwa wamekimbilia katika Miji ya Kaina ,Kirumba n ahata Mjini Butembo.

Tangu juma pili wajaeshi wa Congo FARDC walio rudi nyuma wameonekana kwa mara nyingine kuanzisha mapigano makali na kuzuia waasi wa M23 kuingia katika Mji wa Kanyabayonga wilayani Lubero ambao ni muhimu kwa eneo kwa mkoa wa Kivu Kaskazini .

Wakaazi wakiwa kwa sasa bila msaada kwenye vijiji mbali mbali.

Jeshi la serikali kwa upande wake litikitumia silaha nzito kuwatimua waasi wa M23 kwanye milima mirefu ambako M23 ilikuwa imekita kambi karibu na Mji wa kanyabayonga .

Kanyabayo ikiwa na sehemu mbili ,moja upande wa Rutshuru na nyingine upande Lubero.

Mjini kukibaki watu wachache hasa vijana na wazee wasio jiweza.

AM/MTV News DRC