Shirika la kiraia eneo la Kanyabayonga lasema waasi wa M23 wameendesha mkutano wa hadharani na wakaazi katika Mji wa Kanyabayonga na luofu ,wakiomba wakaazi kurudi nyumbani kwao na kuendelea na shughuli zao za Maisha.
Baadhi ya wakaazi walionekana wakipiga makofi kwa hofu ,Vijiji vikiendelea kutekwa na waasi wa M23 wilayani Lubero baada ya Rutshuru,kama Luofu ,waasi wakiendelea kupambana na waasi wa M23 katika Mji wa Kaina alieko kati kati ya Kanyabayonga na Luofu eneo ambazo kwa sasa zipo mikononi mwa M23.
Wakaazi wa Miji ya Kirumba na Kayna wakiripoti visa vya wizi na uporaji wa mali ya watu ,wafanya biashara katika Mji wa Kirumba wakiomba serikali kuwlainda rai ana mali yake ,Vita vya M23 na jeshi la serikali vime sababisha watu wengi kuhama mkaazi yao na kuwa wakimbizi wa ndani ya taifa lao.wakaazi wakiomba amani na usalama ili warudi kwenye vijiji vyao.
Hadi sasa Mapigano bado ikiripotiwa katika eneo mbali mbali hasa wilayani Lubero,wakaazi wa Miji ya Butembo na Beni wakiwa na hofu Zaidi ,wengi wao wakiwa wafanya biashara na wengine wakiwa wakulima.