DRC

MAPIGANO MAKALI KATIKA MJI WA SAKE KIVU KASKAZINI MASHARIKI MWA DRC.

FEBRUARI 13, 2024
Border
news image

Wakaazi wa Mji wa Sake wote wamekimbia na kuhama makaazi yao katika Mji wa sake kifatia mapigano makali inayoendelea kati ya M23 na jeshi la serikali ya Congo FARDC wanao shirikiana na wazalendo wakaazi hao wasema sababu kubwa yao kukimbia makaazi yao nikuona bomu toka upande wa waasi wa M23 zinaangukia nyumba za watu.

Wanajeshi wa serikali tulio zungumuza nao wasema mapigano ni makali hasa wakishuhudia Mizinga kutoka upande wa waasi wa M23 kwenye milima inayo zunguuka Mji wa sake zaanguka kiholela katika Mji wa Sake na Mubambiro karibu na Kambi ya wakimbizi ya Kamuronza.

Mji wa Sake unao patikana kilometza Zaidi ya ishirini magharibi mwa Mji wa Goma pambeni ya ziwa Kivu nae neo linguine mbuga la Wanyama pori la Virunga ,Sake ni Mji muhimu kwa Goma kwani ni njiapanda yenyi kugawa barabara yenyi kulekea Kichanga wilayani masisi,Minova na vile mushaki kuelekea walikale ,mapiganao katika Mji huo ina hasara kubwa kuhusu chakula inayo toka Minova Kuto fikia kwa mara nyinginee wakaazi wa Mji wa Goma.

Waziri wa Ulinzi Jean Pierre Bemba amsema Mji wa Sake na Goma haitakubalika kuanguka katika Miko ya waasi wa M23 ,akizungumuza na wanahabari kunako uwanja wa ndege wa Goma Bemba amesema serikali ya Congo haitakubali M23 kuingia Sake japo kuwa mapigano bado yako katika Mji huo .

M23 imekuwa ikiomba mazungumuza na serikali ya Kinshasa lakini Kinshasa ikisema haiwezekani kwani ni Rwanda inayo vaamia ardhi ya DRC.Kwasa DRC inashirikiana na SADEC kutwangana na waasi hao kwenye milima ,kikosi kutoka Tanzania kikitumia Mizinga kushambulia ngome za M23 .hadi jioni hii ya juma nne wasiwasi bado yaenelea kwa wakaazi wa Mji wa Goma kufatia mapigano hayo makali.

AM/MTVĀ DRCONLINE