DRC

Mapigano makali kati ya M23 na jeshi la serikali yaendelea wilayani Lubero na Rutshuru Kivu Kaskazini mashariki mwa Congo

JUNI 28, 2024
Border
news image

Wakaazi wa Mji wa Kanyabayonga wasema milio ya silaha nzito imesikika eneo mbali mbali zinazo zunguuka Mji wa Kanyabayonga wilayani Lubero na eeneo la Miriki .wakaazi wakilalamikia bomu kutoka upande wa M23 kuanguka makaazi ya watu katika kata mbali mbali kanyabayonga na Kirumba Pamoja na Luofu.

Waasi wa M23 wamechukuwa vijiji viwili Muhimu wilayani lubero ikiwemo ,Kimaka na Miriki baada ya mapigano makali kati ya FARDC ikishirikiana na wazlendo ,hali ambayo imezusha wasiwasi kubwa na wakaazi kuhama nyumba zao wengi wakikimbilia porini katika misitu kuhofia Maisha .

Waziri mkuu wa Congo Judith Suminwa amesema serikali haita kubali mazungumuzo na waasi hao ama na Rwanda iwapo Rwanda haija ondoa wanajeshi wake kwenye ardhi ya congo DRC ambako Rwanda imekuwa ikikanusha taarifa za kuwepo kwa wanajeshi wake mashariki mwa Congo na sehemu nyingine Rwanda ikisema imekuja DRC kuwatafuta wapiganaji wa FDLR ambao wako kwenye misitu ya congo.

Jumhia ya kimataifa imeomba Rwanda na DRC kutatua mzozo wake kidiplomasia kuliko vita vya maneno na silaha kwani mzozo huo unaweza sababisha vita kote kanda ya maziwa makuu.

Wakaazi wa mashariki mwa Congo hasa wakiu kaskazini wakiomba amani na usalama ili warudi kwenye vijiji vyao.

AM/MTV News DRC