DRCONGO

MAPIGANO YAENDELEA KARUBA MASISI KIVU KASKAZINI Mashariki Mwa DRC

news image
AM
JANUARI 30, 2024
Border
news image

Nchini DRC wakaazi wa Masisi, Rutshuru na Nyiragongo waomba Rais Félix Tshisekedi kushinikiza matendo na maneno

Baada ya Uchaguzi ulio pita wakaazi wanao taabishwa na mapigano inayoendelea kati ya M23 na jeshi wazalendo wanao saidiwa na jeshi la serikali waomba Félix Tshisekedi kuwapa Amani na usalama kwani sasa mashambulizi yamedhidi eneo lao hasa makaazi yao yakishambuliwa kwa bomu toka pande za M23.

Wengi wakisema wamepoteza watu, vitu na wengine wakibaki kambini kwasasa katika hali Duni ya kutatanisha.

Serikali ya kivu kaskazini kupitia waziri wa kiutu muheshimiwa Prisca Kamala Luanda ametembelea waathirika wa bomu zilizo vurumishwa na M23 na kuwaua na kuwajiruhi watu katika Mji wa sake unao patikana kilometa zaidia ya ishirini magharibi mwa Mji wa GOMA.

Hadi tukienda hewani mapigano bado yaendelea kwenye milima ya karuba na mizinga kuvurumishwa eneo za Mushaki maghabi mwa Mji wa sake. Wasiwasi bado ikiendelea. Shirika za kiraia zikiomba SADEC kusaidia kwa haraka jeshi la DRC kuwafukuza waasi wa M23,na M23 kwa uapnde wake ikisema haitaendelea kuvumilia shambulizi za jeshi la Congo wanacho kihitaji waakaazi ikiwa ni Amani na usalama kwakumaliza vita vya muda mrefu mashariki mwa DRC.

AM/Mtv online