DRC SAKE AND KIBUMBA

MAPIGANO MAKALI YARIPOTIWA KATI YA M23 NA JESHI LA SERIKALI FARDC PEMBEZONI MWA MJI SAKE WILAYANI MASISI KIVU KASKAZINI MASHARIKI MWA DRC .

FEBRUARI 12, 2024
Border
news image

Akizungumuza na MTV DRC ONLINE Isamael mkaazi wa Mji wa Sake wilayani Masisi asema kwa sasa hali ni mbaya na wakaazi wachache walio kuwa wamerudi katika Mji wa Sake wamelazimika kukimbia kwa mara nyingine makaazi yao kuhufia usalama kutokana na bomu zinazo dondoka hap ana pale na kuwajiruhiwa watu hasa wanawake na Watoto na wazee wasio jiweza.mapigano ambayo imepelekea familia nyingi kuishi katika hali ngumu katika baadhi ya kambi za wakimbizi.

Mji wa Sake ni Muhimu kwa usalama wa Mji wa Goma ,ikiwa kilometa Zaidi ya ishirini,jeshi la Congo FARD. Limelazimika kutumia helikopta na ndege za kijeshi kujaribu kusimamisha uasi huo wa M23 ambao serikali ya Kinshasa inasema unaungwa Mkono na Taifa jirani la Rwanda ,wakaazi wakisema katika wapiganaji wa M23 kuna vile raia wa Uganda ambao wana saidia uasi wa M23 kuchukuwa vijiji.

Mji wa Goma kwa sasa ukiishi wasiwasi Kubwa japo serikali inaendelea kutangaza kwamba inapambana na waasi hao.Rais wa Congo Felix Tshisekedi alisema hakuna mazungumuzo yoyote na waasi wa M23 ambao wanaungwa Mkono na Rwanda ,Rwanda ikikanusha kilama uungwaji mkono wa waasi hao wa M23 ambao MONUSCO ilisema wana silaha lkubwa . Wakaazi katika Mji wa Sake wilayani Masisi wamezuia leo hii kikosi cha MONUSCO kuelekea uwanja wa mapigano kwa tuhuma kwamba MONUSCO imekuwa ikisaidia M23 na kuzuia jeshi la Congo na Wazalendo kutwanagana na M23 .

Mapigano kati ya M23 na jeshi la Congo imepekea watu wengi kuwa wakimbizi wa ndani wakiishi Maisha maugu bila msaada. .kwa sasa kuna vikosi vingi katika Mzozo wa DRC ikiwemo SADEC,MINUSCO,Na wapiganaji wengine kutoka Ualaya ambao ni wakufunzi wa jeshi la DRC wanao kwenda kwenye mapigano moja kwa moja . Waziri wa Ulinzi wa Congo jean Pierre Bemba alisema Mji wa Goma haiwezi kutekwa na M23 .
AM /MTV DRC ONILINE