DRC

Makundi ya wapiganaji wazalendo mashariki mwa Congo yashutumu mataifa inayo unda umoja wa Nchii za ulaya (EU) kuwa chanzo na msingi wa Vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kuwatesa raia wa DRCongo

JULAI 31, 2024
Border
news image

Akiziungumuza na ITV katika Mji wa Goma Generali Dominique Kamanzi Ndarutse ..mmoja wa Makamanda wa makundi ya wazalendo Kivu Kaskazini mashariki mwa Congo ashutumu Umoja wa nchii za Ulaya EU kuwa chanzo cha mzozo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ndio sababu amekuwa Miongoni mwa watu walio wekewa vikwazo na EU mwishoni mwa wiki ilio pita.

Dominique Kamanzi amesema hata tishika na vikwazo kutoka umoja wa nchii za ulaya kwani alichukuwa silaha kupigania ardhi yake n ahata pesa katika Bengi ama ulaya ambazo zitachukuliwa na EU.

Dominique hata hivyo ameshutumu umoja wa nchii za ulaya kuwa chanzo cha machafuko mashariki mwa Congo kuta kuigawa DRC,ndio sababu ulaya imemuwekea vikwazo kuona kwamba amekuwa miongoni mwa watu wanao zui kuigawa DRC .

Hii ikiwa i siku chache baada ya Umoja huo wa Ulaya kuwawekea vikwazo makundi ya waasi mashariki mwa Congo ikiwemo M23 na hata makamanda ya wazalendo kwa tuhuma mbali mbali ikiwemo ubakaji mateso kwa wananchi na utekeji nyara na ukiukwaji wa haki na msingi za binaadamu .

Umoja wa nchi za ulaya umetangaza vikwazo vyake baada ya Marekani kuwikea vikwazo Viongozi wa AFC yake Corneil Nanga na M23 yake Sultani Makenga na Bertran Bisimwa .Marekani ikiomba pande zote kusitisha mapigano na kwenda kwenye mazungumuzo kwakutatua shida mashariki mwa Congo.

AM/MTV News DRC