DRC

Makabila mbali mbali Kutoka mikoa ya Kivu ya zamani yaombwa kujenga umoja na kusameheana kwa ajili ya uwepo wa amani na maridhiano

AGOSTI 13, 2024
Border
news image

Akizungumuza na wawakilishi wa makabila mbali mbali Mjini Goma PETER CIRIMWAMI gavana wa Kivu Kaskazini aomba makabila yote kutafuta njia nzuri ya kumaliza tafauti zao kwa njia ya maridhiano na mazungumuzo kwa ajili ya amani na usalama.

Cirimwami ameomba haswa kabila na Nande na Hutu kuweka tafauti zao mbali na kuishi Pamoja kwa ajili ya umoja na maendeleo Kivu Kaskazini ,hii ikijiri baada ya makabila hayo kuwa na tafauti kutokana na visa visivyo wapendesza wengine .

Baada ya mkutano muhimu ulio fanyika kunako ofisi za Gavana wa Kivu Kaskazini makabila kutoka mikoa ya zamani imekubaliana kushirikiana na kujenga umoja kwa ajili ya usalama na maendeleo muhimu kwa eneo la Mzozo la Kivu Kaskazini .Mwamo Lebo kutoka nyiragongo akisema eneo lake lina wapokea watu wote na kupongeza pande zote zilizo shiriki mazungumuzo ya maridhiano kuendelea kushinikiza wanawake wazee na vijana wa Kivu Kaskazini kujenga umoja.

AM/MTV News DRC