DRC

Mahakama ya kijeshi ya Butembo ya wahukumu askari 25 wa FARDC adhabu ya kifokwakimbia mapigani dhidi ya M23

news image

Mahakama ya kijeshi ya Butembo, huko Kivu Kaskazini, iliwahukumu wanajeshi ishirini na watano (25) wa Kikosi cha Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FARDC) adhabu ya kifo Jumatano Julai 3, 2024.kwa makosa ya kukimbia mapigano ya M23 na kupora mali ya raia.

Wanajeshi hao walitoroka mustari wa mbele wa Mapigano na kupira mali ya wana vijiji hasa kijiji cha Alimbongo, mahakama hii iliwashutumu askari hawa wa Kongo kwa “kuteketeza silaha za kivita; kukimbia kutoka kwa adui; ukiukaji wa maagizo; nk), kulingana na ACP.

Mbali na wale walio hukumiwa kifo, vipengele vingine 2 vya FARDC vilipokea miaka 10 ya utumwa wa adhabu kwa "wizi".yaani wanajeshi walio husika katika wizi na uporaji wa Mali ikiwmo mbuzi na vitu vya duka akisema Kakule Bozi wa shirika la raia pa Alimbongo.

Bozi ameambia MTV News DRC kwamba walio ibwa vitu na mali ya watu ni wengi ila ameshangazwa kuona 25 ishirini ndio wamehukumiwa baada ya wengine kukimbia.

Wakati wa kesi hii, wanawake wanne, wenzi wa askari, waliachiliwa kwa misingi kwamba uhusika wao katika ukweli hauja thibitishwa, ilionyesha taarifa kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini na Luteni wa pili Reagan Mbuyi Kalonji,

Msemaji wa Fardc wa Operesheni za Northern Front.

Thery Kasereka kwa upande wake ameomba serikali kuwalipa fidia wakaazi walio poteza mali yako kwa sasa Mji wa Alimbongo hauna tena mali na vitu vyote viliporwa .

Kasereka anasema nivigumu kwa wakaazi kwa sasa kurudi tena nyumbani kwao kuona jeshi tiifu kuwapora mali yao.nakuomba wakuu wa serikali kuwajibika na kulipa mali ya wananchi wa Lubero.

Daniel Muhindo - AM/MTV News DRC