Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mheshimiwa FĂ©lix Tshisekedi tangu jioni ya Jumatano Oktoba 30, 2024 awasili jijini Bujumbura, mji mkuu wa jamhuri ya Burundi. Hii ni kwa ajili ya kushiriki katika mkutano wa 23 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) unaofunguliwa Alhamisi hii, Oktoba 31, 2024 jijini BINJUMBURA.
Ziara hii ya rais wa drc yakuja ma saha machache baada yakukutana mwenzake wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mjini Kampala ambapo wakuu hao wawili wa nchi walijadili tathmini ya operesheni ya pamoja kati ya majeshi ya FARDC ya DRC na UPDF katika kuwasaka ADF Mashariki mwa DRC. , Rais wa Jamhuri alielekea Burundi ambako alipokelewa na Mkuu wa Nchi Evariste Ndahishimire.
Ikumbukwe kwamba katika ziara yake mjini Kampala, Tshisekedi alijielekeza na Mkuu wa wa jeshi la congo FARDC na mawaziri wa serikali kuu, hii inakuja mwezi mmoja baada ya mkutano wa kamanda wa sekta ya Sukola 1 na wa Ituri, majenerali Bruno Mandevu na Nyembo Abdallah pamoja na kamanda wa majeshi ya nchi kavu ya Uganda ambao wakati wa mkutano wa tathmini mwishoni mwa Septemba mwaka jana mjini Kampala walikuwa wameamua juu ya kuendelea kwa ushirikiano kati ya majeshi hayo mawili.