DRC/LUCHA

Lucha na makundi mengine waomba serikali ya Congo kumfukuza Balozi wa Marekani na Ulaya nchini DRC kwa tuhuma za unafiki kuhusu vita mashariki mwa Congo

FEBRUARI 19, 2024
Border
news image

Wakivaa mitambaa vyekundi vijana wa Lucha na makundi menngine wamefanya maandamano ya safari ndefu Ilio itishwa na Lucha Pamoja na shirika za Kiraia waendeshaji pikipiki ,Vijana Mjini Goma ,Manadamano ambayo ilikuwa na lengo la kupinga ukimia wa serikali ya Marekani na Ulaya kuhusu uvaamizi wa ardhi ya Congo na Taifa Jirani Kupitia M23 Akisema Aspirine mmoja wa waandamanaji.

Nadia yeye ni msichana na mwanaharakati wa Lucha amesema kwa sasa wamechoshwa na ukimia wa Marekani na Ulaya ndio sababu wamelazimika kuchoma bendera zao kama halama ya kuonesha hathira ya wananchi wa Goma,Masisi,Rutshuru Nyiragongo na mkoa mzima .Vijana walivalia vitambaa vyekundi wakiandamana kwa amani bila uchokozi wowote wametembea kilometa Zaidi ya Kundi kwa Mguu wakiwa na nia ya kuelekea kwenye uwanja wa mapigano katika Mji wa Sake .kwa dakika zamwisho wakaamua kuhitimisha maandamano yao kuepuka Vurugu karibu na Vyombo vya usalama hasa wanajeshi ambao wapo karibu na uwanaja wa mapigano pa Mugunga.

Wakibemba mabango na kuvaa vitambaa vyekundi vijana na wasichana wameshutumu mataifa Jirani wa Congo kuwa wanafiki hasa wakitaja Rwanda na Uganda .

Nadia Nyamusia ni msichana mwana harakati wa Lucha Goma asema Damu ya raia wa Congo imemwagika sana lazima wanao husika kufikishwa ICC hasa Viongozi wa serikali ya Rwanda ambao hujificha katika M23 .

Vyombo vya polisi vilionekana sehemu nyingi Mji Goma kila njiapanda wakiwa na silaha za Moto na wengine wakiwa bomu za kutoa mchozi lakini hakuna tatizo lolote lilo tokea hadi maadamano hayo yamehitimishwa kwa saa za Mchana japo Duka nyingi zilipnekana zimefunga milango yake.

Wakisoma Ujumbe wao vijana hao wameomba Waziri wa Ulinzi na Mkuu wa majeshi kuja kukaa Mjini Goma Pamoja na wanajeshi kwa ajili ya ulinzi wa Mji wa Goma unao andamwa na waasi wa M23 wakisaidiwa na Taifa la Rwanda na washiriki wake wa Mbali kama vile wa Karibu.huku wakaazi wakisubiri matukio kuhusu mkutano wa Ethiopia.

AM/MTV DRC ONLINE