DRC KISANGANI

Kutembeza Meli Usiku Kwenye Mto Kongo na Kubeba Zaidi ya Abiria, Yapigwa Marufuku

JANUARI 15, 2024
Border
news image

Hatua hiyo imechukuliwa juma mosi baada ya kufurika kwa jito Kongo na kusababisha vifo vya zaidi ya watu miya tatu na uharibifu wa zaidi ya makaazi elfu arobaini pamoja na vituo vya afia na maafa mengine mengi kama ya ripoti wizara inchini ihusikayo na mambo ya kihutu pamoja na kijamii. Mutafahamu ya kwamba maafa haya iliwa asiri Wana nchi wanao ishi katika bonde ya muto Kongo kuanjia Kisangani hadi kuelekeya bonde la Matadi jimboni Congo centrale.

Mutafahamu ya kwamba muto Kongo uliweza kufurika siku zilizo pita hivi karibuni na kuwa acha ma elfu za rahiya bila makaazi na Wengine wajane na mayatima . Hatua hiyo ili chukuliwa na viongozi husika na maswala ya usafirishaji kwenye maji ili kuzuiya mabaya yanayo weza tokea kwenye muto wakati huu mgumu ambao mawimbi na zoruba via endeleya kuripotiwa na kupanda na kushuka kwa maji inayo onekana kwenye muto huo.

Kulingana na ripoti iliyo tolewa na wizara inchini ihusikayo na maswala ya kihutu na kijamii, Rais Felix Antoine Tshisekedi ameamua kwamba lazima wa asirika wa janga hilo wapewe musaada.

Ndiweluvula Bin Mutume - MTV News Online