DRC - Butembo

Kiongozi wa kanisa Katholika la Butembo - Beni, Paluku Sikuli Sikuli Melchisédech, asherekea miaka ishirini na tano tangu alipo tangazwa kuwa Uaskofu wa eneo

AGOSTI 11, 2023
Border
news image

Agosti 11, 2023 misa kubwa ilio imefanyika ka huzuriwa na maelefu ya watu Pamoja viongozi mbali mbali kwenye uwanja wa Itav wa shule ya kikatholika /Butembo mtaa wa Kimemi katika Kivu kaskazini misa ilio somwa nae Kardinali Fridolin Ambongo. Wanasiasa,viongozi wapolisi, wafanyabiashara, vijana wanawake na wahumini wa kanisa katholika walishiriki sherehe hizo kubwa katika tamadunina Imani kubwa kwa Dini yao.

Paluku Sikuli Sikuli Melchisédech ni miongoni mwa viongozi wa kanisa katholika ambao kwa mara kadhaa wamekuwa wakikemea hali mbaya ya ukosefu wa usalama na mauaji ya kinyama inayo fanyika katika eneo lake la Butembo Beni ambako maelfu ya wakristo wake wamesha uwawa na wengine kuhama vijiji vyao na kuwa wakimbizi katika taifa lao ama taifa Jirani la Uganda parokia kadhaa zikiota miti zikiwa hazina tena wakristo kutoka na uasi wa Muda Mrefu unao fatia uhalifu wa kivita

Paluku amekuwa miongoni mwa ma pasta ambao wana Imani kubwa kuwa usalama unaweza patikana iwapo Viongozi watawasikiliza wakaazi na kujali maslahi yao wakiogopa mwenyezi Mungu.

kwa muda mrefu Siku Paluku amekuwa akiendelea kuhubiri neno la mwezi Mungu katika sehemu na vijiji visivyo na usalama kama vile eneo la Mutwanga na sehemu nyingi za Beni akikemea uvaamizi wa ardhi ,na watu wasio julikana wanao jificha nyuma ya waasi wanao waua watu kwa muda mrefu ,Sikuli akisema mauaji inayo fanyika katika Diosesi yake ni vitendo visivyo vumilika na sherti viongozi kuchukuwa hatua na kulinda uzima wa wanadamu kwa mfano wa mwezi MUNGU.

Austere Malivika/MTVNEWS