DRC GOMA

ZAIDI YA VIONGOZI WA NYUMBA KUMI MIA MOJA MJINI GOMA WAHUZURIYA KIKAO KUHUSU USALAMA.

JANUARI 31, 2024
Border
news image

Kikao hicho cha kuzungumzia usalama wa muji kime andaliwa naye liwali wa jimbo la kivu kaskazini. Ni viongozi wa makata, mikoa pamoja na nyumba kumi wahuzuriya kikao hicho. Lengo kubwa la kikao hicho, ni kuona hali ilivio ya usalama mjini Goma licha la hatua mbali mbali za viongozi za kudumisha usalama mjini. Baada ya kupiga doriya ndani ya kata za muji wa Goma, imeripotiwa Kuwepo kwa usalama mdogo.

Ndani ya kata vujovu, imeripotiwa askari jeshi wa G R pamoja na wazalendu kuendesha usalama mdogo eneo hilo juma jana rahiya moja akauawa na askari jeshi moja wa GR na majambazi wenye silaha mikononi na moja wapo akashikiliwa. Na ndani ya kata Majengo majambazi walio muua kijana Baraka Mbanza muvunja hela tayari wameshikiliwa na viombo vya kiusalama mjini. Kwa upande wa kata kasika ili ripotiwa Kuwepo na unyanyasaji wa wakaaji na watu wenye silaha mikononi kutoka kambi ya Katindo kwa saha za usiku na Mabanga ya kusini na kaskazini majumba za watu wa kuuza madawa ya kulevia na kutumiya pombe tangu asubui ya ongezeka na kuwa chanjo cha usalama mdogo eneo hizo.

Eneo la kata kahembe, askari jeshi moja wa GR aliweza kupiga risasi mukaaji moja na kufariki dunia na mara moja askari huyu ali shikwa na wakaaji wa kahembe na huko ndani ya kata hilo kumezalika zehebu moja maarufu Malkiya wa Ubembe ambayo ya onekana kuwa hatari kwa usalama wa muji muji siku zijazo. Ndani ya kata keshero, piya walinzi wa viongozi kaza waendeleya kunyanyasa raiya kwa saha za jioni nakuto heshimu muda wa kuwasili kwa boti kwenye bandari ya kituku na kuheshimu muda wa kuvuka mipaka ya Rwanda.

Baada ya kupiga doriya ndani ya kata Zote mjini Goma imeripotiwa kuendeleya kwa usalama mdogo. Jioni ya hii juma ine, kiongozi moja wa kitongoji ndani ya kata LacVert aliuawa kwa risasi uwanjani mwake na majambazi. Viongozi eneo hilo waomba uchunguzi ufanyike kwa kujua walio sababisha uovu huo.

Mipangilio imechukuliwa katika kikao hicho kwa ajili ya kudumisha usalama mjini Goma na liwali wa jimbo walitoa wito kwa wahuzuriyaji kuishi kwa umoja na kushirikiyana kwa kupambana na mambo ya ukabila kwa ajili ya kujenga taifa Letu.

NDIWELUVULA BIN MUTUME MTV NEWS Online