DRC

Kaseghe Lubero mapigano yakuwa makali Zaidi kati ya jeshi la Congo FARDC na waasi wa M23

JULAI 01, 2024
Border
news image

Baada ya kuteka vijiji na miji mbali mbali wilayani Lubero waasi wa M23 wapambana vikali na jeshi la serikali kwenye kijiji cha Mbasa Vutsorovya wilayani Lubero tangu asubui ,jeshi la Congo likijaribu kuzuia waasi kuendelea kuteka vijiji kila siku.

Bienvenue mmoja wa wakaazi wa Kijiji cha kaseghe asema milio ya silaha nzito imesikika tangu mchana huu katika Kijiji chao na kulazimisha wakaazi kukimbilia porini na kwnye mashamba.Beinvenue anasema kwa sasa wanawake na Watoto wamekuwa na ugonjwa moyo kutokana mirindimo ya risasi kutoka silaha nzito za M23.

Mapigano kati ya M23 na jeshi la serikali imesababisha maelfu yaw ana vijiji kuhama makaazi yao na kuwa wakimbizi wa ndani katika taifa lao ,wengi wao wakikimbia safari ndefu kwa miguu wakibeba mizigo na wengine wakitumia pikpiki na gari kama usafiri wao kuhofia Maisha .

Waasi wa M23 wamesonga mbele Zaidi wilayani lubero baada ya jeshi kushindwa kuwadhibiti kwenye vijiji vya Miriki na kanyabayonga ambako walipigana kwa Zaidi ya mwezi mmoja .wakaazi wanasema mili ya watu wanao dhaniwa kuwa wanajeshi na wazalendo ilionekana katika mji wa kaseghe leo moshi julai elfu mbili ishirini na nne .

Wakaazi wakiomba amani na usalama kwani wamechoshwa sasa na ukimbizi na vita vya kila siku.

AM/MTV News DRC