DRC

Jeshi la wanainchi wa Uganda UPDF la omba wa kaaji wa Butembo na Beni kuwa watulivu

APRILI 2, 2025
Border
news image

Akizungumuza na wakaaji wa kata la furu Mjini Butembo, mmoja wa makamanda wa jeshi la Uganda UPDF asema hakuna hata mwana njeshi wa jeshi lao kutoka Uganda atakae ondoka kwenye mstari wa mapambano wilayaani Lubero, bila amri kutoka kwa uongozi wa nchini Uganda.

Utaafamu kwamba Uganda ina wananjeshi wengi mashariki mwa Congo Kinshasa ikiwemo Lubero, Butembo, Beni na wilaya zake katika musako wamakundi ya waasi ikiwemo ADF na CODECO mkoani Ituri pamaja na kuzuiya kundi la waasi wa AFC/M23 kuingia Mjini Butembo ambako waendelea kuandama serikali ya Kinshasa.

Jeshi la Uganda lasema limekuja nchini DRC hasa eneo lake la mashariki kwa kualikwa na serikali nani muhimu kuendelea kuzingatia makubaliano yao ambayo ni kuwapa amani na usalama wakaazi wa DRC ambao wameandamwa kwa muda mrefu na machafuko ya mara kwa mara hasa mauaji na mashambulizi kutoka kwa watu wanao dhaniwa kuwa ADF ambako washutumiwa kwa mauaji na uhalifu wa kivita.

ADF ni kundi lenye kushikilia silaha ambalo serikali ya Kinshasa ya chukulia kama vile kundi la Kigaidi kutokana na utaratibu wake wakuwauwa wananchi kwa mapanga, shoka, risasi na hata kuwateka wengine na kuwalazimisha kuingia katika kundi lao katika misitu ya Beni ambako hulazimisha kila mtekwa kuwa Muislam.

Kufatia tetesi za kuondoka kwa UPDF wilayani Lubero imesabisha wakaazi wa Butembo kuwa na wasiwasi, wengi wakisema hawana tena imani na jeshi tiifu kwa serikali FARDC, kutokana na kile wanacho shutumu kwamba jeshi hilo lina wanafiki na wasaliti ambao washirikiana na waasi wanao endelea kuchukuwa vijiji wilayani Lubero kivu kaskazini.

Kwa sasa UPDF imeendelea kurundika jeshi lake Iuturi na Beni na kwa sasa Lubero.

AM/MTV News DRC