DRC

Jeshi la Uganda UPDF na FARDC ya Congo yawakamata wapiganaji Zaidi ya tehelathini wa ADF wilayani mambasa Mkoani Ituri

SEPTEMBA 23, 2024
Border
news image

Akizungumuza na MTV akiwa katika Mji wa Biakato wilayani mambasa Fleix Kambale asema muungano wa jeshi la Uganda UPDF na lile la Congo FARDC wafanikiwa kuwaua wapiganaji Zaidi ya ishirini wa ADF na kuwamakata wengine Zaidi ya thelathini hasa wanawake na Watoto.

Walio shuhudia ujio wa helikpta ya jeshi la Uganda wasema helikopta hiyo ilirudi moja kwa moja nchini Uganda na matekwa ambako wanapelekwa katika center ya ki psycholojia kabla ya kurejeshwa katika familia .

Jeshi la Congo FARDC na lile la Uganda UPDF likitangaza kuwakamata wapiganaji Zaidi ya thelathini kutoka Kundi la ADF na wenginezaidi ya kumi kuwawa kuuwawa na silaha zao kukamatwa wakati wa mapigano makali pembezoni mwa Mji wa Biakato katika vijiji vya Mitume,Kasoko,lelesi,Manyama,Mabuho wilayani Mambasa Mkoni Ituri ,Zaidi ya kilometa hamsini maghabi mwa mji wa Beni .

Kambale akiwa ni mkaazi wa Mji wa Biakato ameshuhudia na kuona jeshi la Uganda UPDF ikiwaleta kwa gari za kijeshi wanawake na Watoto na kupanda helikopta hadi Uganda ambako wanapelekwa katika kitengo cha uchunguzi .huku Meja Generali Bruno Mandevu kwa upande wake akipongeza wanajeshi kwa kazi kubwa ambayo waendelea kutekeleza kwenye ardhi ya Congo hasa kujitolea Zaidi kwa ajili ya amani na usalama wa wananchi wa Beni na Ituri ambao wamesha poteza ma mia ya ndugu jamaa na marafiki tangu mauaji kuripotiwa Beni .

Watoto na wanawake wamakamatwa baada ya mapigano makali ambayo imepelekea baadhi ya wanajeshi wa Uganda nao kujeruhiwa .

wanawake wilayani Beni kivu Kaskazini wakipingeza operesheni hizo akisema Noel Muliwavyo .Muliwavyo amesema amehesabu watu ishirini na saba wote wakiwa wanawake na Watoto ambao wameokolewa wakati wa mapigano kati ya UPDF na ADF.

AM/MTV News DRC