DRC

Jeshi La DRC Latangaza Kuzuia Jaribio La Shambulizi La Waasi Wa M23 Katika Kijiji Cha Matembe Wilayani Lubero Kivu Kaskazini

news image

Kwa mjibu yake luteni MBUYI KALONJI REGEAN msemaji wa opereshi eneo la kaskazini mwa mkoa wa kivu kaskazini, Vikosi vya Jeshi la jamhuri ya kidemokrasia ya Congo vinavyo jihusisha na operesheni Kaskazini mwa mkoa atangaza kwamba jeshi la FARDC lime zuia maranyingine majaribio kadhaa za waasi wa M23 na washika wao wa RDF siku nzima ya Jumatatu Desemba 2, 2024 katika kijiji cha MATEMBE na viunga vyake wilayani Lubero Kivu Kaskazini.

Luteni MBUYI KALODJI ameiambia mtv katika barua pepe kwenye mtandao wake waki jamii kwamba vikosi vya FARDC Vilikabiliwa na uvamizi huu ambao ulio lenga kambi zao.

Vikosi hivyo viliwapa pigo na hasara kubwa kwa adui RDF/M23, huku vifo na majeraha kadhaa vilirekodiwa hapa na pale kwenye uanza wa mapigano.

Ilipo timia masaha za jioni ya jumatatu December 2, 2024 RDF M23 ili rusha kwa upofu mabomu mawili ya RLM, ambayo yalianguka kilomita 2 kutoka Hospitali ya Rufaa ya Alimbongo, na kusababisha uaribifu na watu ku kimbia.

Wakijibu milio ya risasi ya waasi hao, FARDC iliendelea kupa kuchapo ma jeshi ya rwanda RDF na M23 ambao kwa hila yao walitaka kuvunja Milima ya Kasinga, na Utwe.

Luteni MBUYI KALONJI aombwa raia kuwa watulivu na kuendelea kuliamini jeshi lao, hapa akihakikisha kwamba jeshi la DRC laendelea ku dhibiti maeneo yote na hali ya usalama.

Germain Hassan Kyahwere, MtvDRC