Muungano ya jeshi la congo FARDC na jeshi la ulinzi la wananchi wa UGANDA UPDF ya tangaza kupokonya Silaha 2 aina Ak 47 na bomu 12 wakati ya mapigano kati ya FARDC-UPDF na waasi ADF-MTM-ISCAP Oktoba 22 hadi 23, 2024 kando kando mwa mto EBIENA, sekta ya BAPERE,wilayani LUBERO kaskazini mwa mkoa wa kivu kaskazini.
MAK HAZUKAY msemaji wa operesheni za kijeshi SOKOLA 1 dhidi ya makundi yenye silaha kaskazini mwa mkoa wa kivu ikiwemo ADF ,asema kwamba waasi wa 2 wametokomezwa na wengine kadhaa kujeruhiwa vikali kulingana na nyayo ya damu ilio onekana kwenye uanja wa vita upande ya waasi wa ADF.
Kumbuka kwamba,jeshi la Congo FARDC na jeshi la ulinzi ya wananchi wa UGANDA UPDF waendelea kujaribu kutokomeza kundu hili la adf katika wilaya ya IRUMU,BENI,MAMBASA na LUBERO mashariki mwa Congo tangu zaidi ya miaka mbili sasa.