Katika tangazo alillo lisoma mbele ya wanahabari Mjini Goma .Luteni Kanali Djike K Gullaume msemaji wa jeshi Kivu Kaskazini asema waasi wa M23 wanao ungwa Mkono na Tiafa jira ikiwemo Rwanda na Uganda. Djike amesema "Tangu saakumi za asubui waasi wa M23 wanao ungwa mkono na jeshi la Rwanda walishambulia ngome zetu nyingi pa Mpati na kusababisha wakaazi kukimbia vijiji vyao ,hii ikiwa ukiukwaji wa makubaliano ya usitishwaji wa Mapigano ilio wekwa na serikali ya Marekani".
Jehsi la Congo limeomba jumhia ya kimataifa kufanya uchunguzi kuhusu uchokozi waw a M23 na wasaidizi wake ambao wazidi kuyumbisha usalama na kupelekea ma mia ya wakaazi kuhama vijiji vyao na kuishi Maisha mabaya hasa Watoto na wanawake ambao kwa sasa waishi Maisha mabaya na wengine wakinyeshewa na mvua kali inayo shuhudiwa kwa sasa.
Tangazo la jeshi la Congo limejiri baada ya M23 nao kutangaza kuwa serikali ya Congo imekeuka usitishwaji wa mapigano wilayani Lubero karibu na Mji wa Kaseghe .Mapigano kati ya M23 na jeshi la serikali imesababisha Maisha ya watu kuwa mbaya zaidi na kupoteza kila kitu Pamoja na uporaji wa Mali.