DRC

Jeshi la Congo FARDC la laumu waasi wa M23 kukiuka usitishwaji wa mapigano kwakuchukuwa Kijiji cha KIKUVO wilayani lubero Kivu kaskazini

AGOSTI 27, 2024
Border
news image

Katika tangazo la jeshi lililo somwa nae Luteni kanali Ndjike Kaiko msemaji wa FARDC Kivu Kaskazni ,jeshi la sema waasi wa M23 wakiungwa Mkono na taifa la Rwanda limeshambulia Ngoma za jeshi tiifu kwa serikali na kukiuka shughuli za usitishwaji wa mapigano zilizo wekwa kwa ajili ya kuendelea na mazungumuzo ya Lwanda.

Ndjike amesisitiza kwamba M23 /AFC na jeshi la Rwanda RDF limepotosha wananchi katika tangazo zake zinazo husu ukiukwaji wa anga zake na ndege za jeshi la DRC.M23 ilisema jeshi la Congo limetumia ndege zake kuruka eneo lake nah ii ikiwa ni ukwaji ,swala linalo tupiliwa mbali na jeshi la serikali.

Wakaazi kwa upande wao wakiomba M23 kusema ukweli iwapo eneo hilo la Congo limekuwa taifa lao na Rwanda kwani ni vigumu kuelewa tangazo lao akisema Laurent mugiraneza .Mugiraneza hata hivyo ameomba serikali kusitisha malalamiko bali kuchukuwa hatua.

Rwanda kwa mara kadhaa imekuwa ikikanusha kwamba haina wanajeshi wake Nchini DRC ,bali wako mpakani kulinda taifa katika kile wanacho kiita kuzuia wapiganaji wa FDLR .

M23 kwa sasa ikiendelea kuchukuwa baadhi ya vijiji wilayani lubero baada ya Masisi.Marekani na Ulaya ikiomba pande zote kwenda kwenye mazungumuzo kuliko kuchochea machafuko na vita ambavyo vya weza zuka kanda ya maziwa makuu.

AM/MTV News DRC