TANZANIA

Idadi ya vifo vinavyo tokana na mauaji ya siku sita Mfululizo wilayani Beni yafikia Zaidi ya miamoja hadi sasa wakisema viongozi wa shirika za kiraia eneo husika

JUNI 06, 2024
Border
news image

Mashirika ya kiraia katika eneo la Mabalako wilayani Beni yasema hali ni mbaya na kuuzunisha kutokana na mauaji mabaya ambayo imeshuhudiwa kwenye vijiji mbali mbali vilivyo shambuliwa na watu wanao dhaniwa kuwa ADF.

Utafahamu kwamba vijiji vya Masala ,Kabweke,Maindoni,Keme,Makusa na kwa sasa idadi ya watu walio fariki Dunia ikiwa Zaidi ya miamoja hadi sasa baada ya mauaji ilio tekelezwa kwa siku tano mfululizo tangu tarehe 4 hada sasa.

Paluku kavalami mmoja wa viongozi wa mashirika ya kiraia eneo husika asema kwa sasa mili 96 tisini na tisa ndio imezikwa huku nyingine ishini na Moja ikiwa bado katika Kijiji cha Mashana ikiwa imeanza kuoza kutokana na hali ya misitu na vijana wanao jitahidi kutafuta maiti wakionekana kuchoka misituni.

Paluku Kavalama anasema hali kwa sasa ni mbaya nay a wasiwasi kubwa ,wakaazi wakilazimika kuhama vijiji vyao na kukimbia Butembo na Beni kunusuru Maisha kutokana na mauaji ambayo ni yakutisha inayo tekelezwa na watu wanao dhaniwa kuwa ADF.

AM/MTV News DRC