DRC

Hali yarudi Tulivu Katika Mji wa kanyabayonga wilayani lubero baada ya mapigano makali ilio pelekea watu nne kujeruhiwa kwa Bomu

JUNI 21, 2024
Border
news image

Mkaazi mmoja katika Mji wa kanyabayonga asema jioni hii hali imerudi tulivu baada ya mapigano ilio anza tangu asubui ya leo juni ishirini na mmoja katika Mji wa kanyabayonga wilayani Lubero ambako watu kwa sasa waishi wasiwasi kufatia bomu zinazo vurumishwa na M23 na kuwajeruhi ama kuwawa wakaazi wasio kuwa na hatia.

Mkaazi huyu anasema wakaazi wachache walio baki Mjini wameanza kufanya biashara na kutembea Katika Mji wa Kanyabayonga japo vitisho vya waasi wa M23 ambao kwa Zaidi ya wiki moja sasa wana twangana na jeshi la Congo likuungana na wapiganaji wazalendo ambao wanajiunga na jeshi la serikali kuzuiz kile wanacho kiita uvaamizi.

Mji wa Kanyabayonga ni Mji muhimu kwa Miji ya Butembo,na Beni kuunganisha eneo la kivu na la kaskazini la Mkoa wa Kivu Kaskazini .Lubero ni wilayani ambayo ina watu wengi mkoni kila Kijiji kiwa na wakaazi wengi ambao kwa sasa waomba serikali ya Kinshasa kutafuta suluhu kwa mzozo wa M23 na serikali ya Kinshasa.

AM/MTV News DRC