DRC SAKE MASISI KIVU KASKAZINI.

HALI YA UTULIVU IMERIPOTIWA KATIKA MJI WA SAKE KILOMETA ZAIDI YA ISHIRINI MAGAHRIBI MWA MJI WA GOMA.

FEBRUARI 14, 2024
Border
news image

Akizungumuza na MTV DRC ONLINE mkaazi mmoja alie kimbia makaazi yake na kwa sasa akiwa amejielekeza katika Mji wa sake unao patikana kunako kilometa ishirini magharibi mwa Mji wa Goma asema ( hapa hali ni kimia ,nimejaribu kuzuunguka kote Mjini sija waona waasi wa M23 najiuliza wako wapi ila kuna hofu kubwa sana,sehemu moja nimeona wapiganaji wazalendo wakiwa na silaha kwenye Njiapanda ya Sake karibu na Station ya Mafuta ,nimefika kwenye soko ya Ngurue nikavuka kamtoni kadogo ,lakini nimerudi nyuma kwa hofu ya kushambuliwa kwani M23 ipo katika Milima inayo zunguuka Mji wa Sake)akisema mkaazi tulie zungumuza nae kwa njia ya simu.

Utafahamu kwamba maelefu ya wakaazi wa Mji wa Sake wote wamekimbilia katika Mji wa Goma kuhufia Maisha hasa kuogopa kuangukiwa na bomu zinazo vurumishwa na waasi kutoka kwenye milima .makaazi ya watu ikiporwa na watu wenye silaha ,milango ikibaki wazi baada ya wenyeji kutoroka na kukimbilia Goma kuhufia Maisha. Mji wa Goma kwa sasa unashuhudia maelfu ya wakaazi kutoka kwenye vijiji wakikimbia vijiji vyao.

Wengi wakiwa bila msaada wa chakula kama vile dawa ,nma wengine wakipokelewa na familia mbali mbali kwenye baadhi ya Kata za Mji wa Goma kama vile ndosho. Naibu Waziri Mkuuu na Waziri wa ulinzi wa Congo jean Pierre Bemba alitangaza kwamba wakaazi wa sake wawe watulivu n ahata wale wa Goma kwani vyomvo vya ulinzi na usalama vya Congo DRC yaani FARDC vimejipanga kuhakikisha Goma inalindwa vilivyo.

Umoja wa mataifa umeshutumu Rwanda kusaidia waasi wa M23 kuwapa silaha za kisasa ambazo ni mbaya na ikiwa tishio silaha ambazo zina uwe wakushambulia ndege sizizo na marubani zikiwa mbali n ahata zile za kivita.

AM/MTV DRC ONLINE