DRC

Hali ya usalama Imerudi Tulivu katika sehemu mmoja ya Mji wa Goma baada ya maandamano makubwa ya wananchi wanao omba usalama wao wakipinga mauaji ya kila siku

AGOSTI 12, 2024
Border
news image

Nibaada ya polisi na jeshi la serikali FARDC kuingilia kati vurugu katika kata la Majengo na Vuhene hali ya Usalama imerudi tulivu na barabara kufunguliwa na vikosi vya polisi wakishirikiana na baadhi ya wananchi walio jitolea kuondosha mawe barabarani.

Wakaazi wa Mji wa Goma na Vuhene wakishutumu serikali kushindwa kuhudumisha usalama hasa kukishuhudiwa mauaji ya kila siku jioni na vitu kuporwa na watu wenye silaha.wakaazi wa kata la Vuhene wakilaumu jeshi na Polisi kushindwa kulinda usalama na kushutumu baadhi yaw ana usalama kuhusika katika ukosefu wa usalama wakipiga wananchi risasi.

Nyiragongo ikiwa na wakaazi wengi imesema vyombo vya usalama kwa sasa vimekuwa tishio kwao baada ya kuwawaua watu walio kuwa katika ibada ya mafarijiji na kuwaua watu wa tatu na wengine tano kujeruhiwa na askari jeshi tiifu kwa serikali.

AM/MTV News DRC