DRC

Hali imerudi Tulivu kwenye mpaka mdogo unao igawa DRC na Rwanda unao julikana kama petite Barierre , baada ya mlio wa risasi kusika mpakani na kuwajeruhiwa watu ambao idadi yao haijulikane hadi sasa

AGOSTI 29, 2024
Border
news image

Akizungumuza na Christian Kalamo wa shirika la raia mtaani Karisimbi, asema kuwa uchunguzi kwa sasa unafanyika na viongozi wa Mji wa Goma.wachambuzi wa mswala ya kiusalama kwa upande wao wakisema hii ikiwa halama na ujumbe kwa watu wanao wasaidia waasi wa M23 kiuwa wananchi wa Congo wamechoshwa na Vita vya uvaamizi kutoka kwa mataifa Jirani.

Walio shuhudia mfarakanyiko huo wakisema kuna majeruhi ambao kwa sasa idadi yao haijulikane hadi sasa kwa pande zote. Vyombo vya usalama vikiendelea na uchunguzi ila mutu mmoja anae shukiwa kuwa mzalendo kukamatwa kuwa na kwa sasa akiwa mikoni mwa vyombo vya usalama Mjini Goma.

Hali hii ikileta wasiwasi kubwa ,huku Rwanda na DRC ikijaribu kutafuta suluhisho la Pamoja kutafuta mani na usalama kanda ya maziwa makuu na kukomesha vita mbavyo vimepelekea maelfu ya watu kuwa wakimbizi katika taifa lao na kusababisha DRCongo kupokea vikosi vingi.

Mjini Goma kukiwa wanajeshi wa Umoja wa Matifa MONUSCO, SADC kwa upande mwengine, jeshi la Congo FARDC vijana wazalendo na wengine.lakini mji huo kwa sasa ukishuhudia hali mbaya ya kiusalama katika Mtaa wa Karisimbi kukishuhudiwa risasi kila jioni na uporaji wa mali usiku ukitekelezwa na watu wenye silaha.

AM/MTV News DRC