DRC GOMA

GAVANA WA KIVU KASKAZINI ASHIKA KASI KATIKA MIRADI YA MAENDELEO HASA UJENZI WA BARABARA MUHIMU MJINI GOMA.

FEBRUARI 28, 2024
Border
news image

Meja Generali PETER CIRIMWAMI afanya uzinduzi wa kazi za ujenzi wa lami kwenye baadhi ya njia zinazozunguka jengo la mahakama ya Goma leo hii Februari 28, 2024. Ikiwemo njia za Myakano ambazo zitaboreshwa na kujengwa kwa lami wakisema wakuu wa kambuni ya ujenzi ya Kongo SOCOC kwa kifupi. Timothee sangwa Sumaili ni mkurugenzi wa ofisi ya barabara na mifereji ya maji anaelezea mradi huu utatumia pesa za marekani dola $584,722 bila kujumuisha kodi, mradi huo tafadhiliwa na serikali ya mkoa wa Kivu Kaskazini.

Hii ikiwa kuendelea na juhudi za Rais wa taifa FELIX TSHISEKEDI kuweka amani , maendeleo na mabadiliko chanya. Gavana wa kijeshi wa Kivu Kaskazini, Meja Jenerali Peter Cirimwami Nkuba alifichua faida za mradi huu katika kuboresha hali ya maisha.

Huku walengwa wakiwa na furaha kwa ujenzi wa Miradi hii ya maendeleo hasa wakaazi walio shuhudia uzinduzi wa muradi huu mkubwa kwa saa za asubui wakati kuna mapigano wilayani masisi ikiwa sio mbali na Mji wa Goma. Baada ya kukagua maeneo ya ujenzi na nyumba zilizokwamisha barabara kuu ya umma, Meya wa Mji asema makaazi ilio jengwa barabarani itabomlewa na kuangushwa chini.

Mkuu wa mkoa hata hivyo alitembelea eneo la mahakama ya Goma ambapo alipendekeza uboreshaji fulani na kuonesha ujenzi wa majengo mengine .

AM/MTV