DRCONGO

DRCONGO PITER CIRIMWAMI GAVANA WA KIVU KASKAZINI APATA SULUHISHO KUHUSU MZOZO KATIKA SOKO KUU YA KITUKU MJINI GOMA.

FEBRUARI 22, 2024
Border
news image

Akitembelea wafanya biashara Katika soko ya Kyeshero haswa katika soko kuu ya Kituku, hii tarehe 22 Februari , 24, mkuu wa mkoa Meja Generali Piter Chirimwami amekutana na wafanyabiashara na wawakilishi mbalimbali wa wakazi kujadili kuhusu kodi ya wanamazingira inayopingwa na wakazii pamoja na usalama tete katika sehemu hii ya Goma.

CIRIMWAMI amesema wafanya biashara wa Mkaa wataenelea kulipa kodi yao ya kawaida ikiwa ni franga mia tano (500 FC ) namna walivyo kuwa wakilipa ,pamoja na kuwachukulia hatua watumiaji wa Boti ambao hawana Life Jackets Kwa ajili ya ulinzi na usalama wa Abiria katika ziwa Kivu .kuhusu usalama serikali ipiga marufuku usafiri wote kuanzia saakumi na Moja ama kuingia saakumi na Moja haitakubalika

Hatua nyingine nikupiga marufuku kodi zisizo julikana na serikali zinazo tozwa na watu wa usalama, muuzaji wa mkaa akikaribisha harakati za mamlaka kukutana na waa wafanya biashara wa Soko kuu ya Kituku. Amesema GAVANA wa Kivu Kaskazini Piter Cirimwami amefanya kazi kubwa kutatua kero yao kwa haraka

baada yakuwasikiliza wakaazi pamoja nna watumiaji wa Soko ya Kituku Mjini Goma ambako amefanya mazungumuzo ya kina Suluhisho kadha zimechukuliwa na mkuu wa Mkoa kwa kuridhika wa wafanyabiashara kupitia uongozi wa utawala wa ndani wa serikali ya mkoa wa Kivu Kaskazini.

Mkuu wa serikali na Muwakilishi wa Rais wa Taifa la Kivu Kaskazini Meja Jenerali Peter Cirimwami atoa maagizoKadhaa kwa kumaliza uhasama kati ya wananchi na serikali hasa wafanya biashara kuhusu unyanyasaji walio kuwa wakilalamikia .Gavana amesema kwa sasa ni marufuku kutumikisha ambao hawana mamlaka kwenye bandari bandarini.

AM/MTV DRC ONLINE