DRCONGO

GAVANA WA KIVU KASKAZINI PETER CIRIMWAMI AOMBA WAKIMBIZI KATIKA KAMBI MBALI MBALI KUWA WAVUMILIVU KWANI HIVI KARIBUNI WATARUDI KWENYE VIJIJI VYAO.

FEBRUARI 23, 2024
Border
news image

Akizungumuza na MTV DRC ONLINE Gavana wa Kivu Kaskazini Meja Generali PITER CIRIMWAMI aomba wakaazi wote Pamoja na wakimbizi wanao patikana katika kambi mbali mbali mashariki mwa Congo kuwa watulivu kwani hivi karibuni watarudi kwenye vijiji vyao kufatia jitihada zinazo fanya na serikali ya Congo kupitia FELIX TSHISEKEDI. CIRIMWAMI alisema hali ya wakimbizi ni mbaya kambini kote pembezono mwa Mji wa Goma kwa sasa kinacho hitajika na mashirika mbali mbali kuweka nguvu Zaidi kusaidia wakimbizi kwa vyakula,Dawa na mavazi .

Wakimbizi hao wengi wakiwa nikutoka wilayani ya Masisi ,Rutshuru na nyiragongo ambako walikimbia Vita vikali kati ya M23 na jeshi la serikali FARDC na upande mwengine na wapiganaji Wazalendo ambao kwa muda mrefu watwangana na M23 wilayani Masisi. Baadhi ya wakimbizi wasema hali ni Ngumu .

(( Yvette Jean Dedieu ni mmoja wa akina mama wakimbizi katika kambi ya Bulengo magharibi mwa Mji wa Goma asema kwa sasa wana kosa vitu vingi sana ikiwemo Tiba yaani dawa,Chakula na huduma muhimu kwa wanawake wanacho hitaji nikuona malalamiko yao inafikishwa kwa Rais wa Taifa la Congo DRC ili warudi nyumbani kwa sasa wanacho kihitaji haraka ikiwa ni chakula ))

Katika baadhi ya kambi utawakuta Watoto wakiwa wamepoteza uzito wao n ahata kugeuka rangi kutokana na utapia Mulo unao waandamana,wazazi wakisema walipoteza Watoto wao wakati wa Vita vya shasha hadi sasa wamejitenga na familia kutokana na vita mashariki mwa CONGO.

Mkimbizi mmoja alie hifadhi jina lake anasema anashangazwa kuona mutu mmoja ameharibu Maisha ya mamilioni ya wakaazi wa mashariki mwa Congo kwa maslahi yake Binafsi ,wakitaja Rwanda Moja kwa moja. Rwanda imeshutumiwa na serikali ya Congo na mashirika mengine kuwa imekuwa katika uhalifu mashariki mwa Congo ikiendelea kuunga mkono kundi la waasi wa M23.

Wachambuzi wa mashwala ya kiusalama wanasema vita mashariki mwa Congo vya weza zagaa katika kanda ya maziwa makuu iwapo njia za kidiplomasia hazita chukuliwa kwa haraka kwani katika vita hivyo kuna wadau wengi wanao jificha nyuma ya M23 .

AM/MTV DRC ONLINE