DRC

Felix Tshisekedi wa Congo afungua Rasmi Mjini Kinshasa mkutano Muhimu kuhusu usalama na uongozi wa kijeshi Kivu kaskazini na Ituri

AGOSTI 14, 2023
Border
news image

Katika hutuba yake mbele ya wajumbe kutoka mikoa mbali mbali ,baadhi ya wabunge,seneta,wawakilishi wa mashirika ya kiraia,na wajumbe kutoka serikali kuu Mjini Kinshasa, Rais wa DR Congo asema kuwa wabunge wa kivu kaskazini na la ituri Pamoja na wajumbe kutoka serikali wata fikiria ku husu uongozi wa dharura kwa muda wa siku tatu na kuamua ujio wa Mikoa ambayo inakabiliwa na machafuko ambako viongozi wake ni wanajeshi.

Felix Antoine Tchisekedi amesema kua hatua ya kuweka uongozi wa kijeshi mkoani Ituri na Kivu kaskazini nikutokana na hali mbaya ya usalama inayo sababishwa na makundi yenye silaha inayo tatiza wakaazi wengi mashariki mwa Congo na kusababisha wengi kuwa wakimbizi wakiacha makaazi yao wakihufia Maisha kutokana na mauaji ya kinyama ya mara kwa mara.

Utafahamu kwamba ni tangu tarehe 6 may 2021 ndipo Rais wa Kongo Felix Tchisekedi ali tangaza uongozi wa dharura katika mkoa Kivu Kaskazini na Ituri ambako kuli wekwa uongozi wa kijeshi hadi sasa akiwa na lengo la kurejesha Amani na usalama .wengi wakiomba kurejesha uongozi wa kiraia na wengine wakiomba uongozi wa kijeshi kubaki.

MTV NEWS