DRC

Familia za waandamanaji walio Waathirika wa MONUSCO miaka miwili ilio pita Butembo na Beni Waomba makaamanda wa UN nchini DRC kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya raia

JULAI 30, 2024
Border
news image

Familia za waandamanaji walio uwawa na vikosi vya umoja wa mataifa MONUSCO miaka miwili ilio pitaka katika Miji ya Butembo na Beni waomba makaamanda wa UN nchini DRC kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya raia wa Congo DRC.

Akishiriki adhimisha ya miaka miwili ya kumbukumbu ya mauaji ya vijana wa Mji wa Butembo na kikosi cha Umoja wa Matifa MONUSCO Rose Kahambu Tuombeane mwana harakati wa kutetea haki za wanawake na Watoto katika mji wa Butembo Kivu Kaskazini asema wakaazi wa Butembo tarehe ishini na sita wanakumbuka vijana Zaidi ya kumi na Tano walio uwawa na vikosi vya Umoja wa Mataifa MONUSCO katika Mji wa Butembo na Kasindi wilayani Beni.

wengine zaidi kumi kujeruhiwa kwa risasi walipo kuwa wakiomba MONUSCO kuondoka nchini DRC kwakushindwa kulinda raia.Wazazi wengi wakiomba makamanda wa Umoja wa mataifa monusco kufikishwa mahakamani na kulipa fidia Watoto wao akisema Kahambu Kwira Twiwe mmoja wa wazazi miongoni mwa wangine walio poteza Watoto wao kwakupigwa risasi wakati wa maandamano Julai elfu mbili ishirini na mbili pa Kavitero Butembo.

Wengi bado wakiwa hawaja farijika hadi sasa baada ya Watoto wao kufariki Dunia kwa ajili ya Kupinga uwepo wa MONUSCO Nchini Congo DRC .Siku chache baadae MONUSCO ili lazimika kuondoa ofisi zake Butembo baada ya maandamanao ilio fanya Zaidi ya wiki moja kukiwa vifo na majiruhi kwa wakaazi.

Hadi sasa serikali ilitangaza vifo Zaidi ya thelathini kote kivu Kaskazini kutokana na maandamano hayo katika Mji ya Goma,Butembo,Beni na Kasindi.kwa sasa MONUSCO wakiwa wamesha ondoa ofisi zao katika Mji wa Butembo kufatia ombi na malalamiko ya wakaazi .familia bado zikisubiri hatua ya Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji walio tekeleza dhidi ya Raia wa Congo.

AM/MTV News DRC ONLINE