Katika mkutano na wanahabari Mjini Kinshasa Mji mkuu wa Congo DRC ,Msemaji wa serikali Patrick Muyaya pamoja na Serge Tshibangu wasema maandalizi ya kuwapokea wageni kutoka eneo mbali mbali na inje ya inchi yanakwenda vizuri .
Vyombo vya usalama ikiwemo jeshi ,polisi na wengine wamewekwa kila sehemu akisema Anicet Sekimonyo mwanahabari alieko eneo hilo .Hata hivyo msemaji wa serikali ya Congo Patrick Muyaya amesema na haki ya serikali kuwekea watu ulinzi kwani kuna ma mia za watu wanao subiriwa kundoka mikoa na miji mbalimbali ya DRCongo kushuhudia wenyewe kuapishwa kwa rais wao Fleix Tshisekedi .Mizinga sihirini na mmoja itapigwa pamoja na gwaride za kijeshi itashuhudiwa wakati wa sherehe hizo .
Waalikwa kutoka mataifa mbali mbali wanasubiriwa ikiwemo Rais wa Burundi na ujumbe kutoka serikali ya Kenya na hata serikali ya Marekani ,Mji ukishuhudia mapambo kila sehemu hasa barabara zenyi kutoka uwanja wa ndege hadi Mjini .
Wakati huohuo upinzani nao umetangaza kuandamana hapo kesho kama halama ya kupinga uchaguzi ulio fanyika decemba iliopita.Muyaya amesema DRC ni taifa la Kidemokrasia ila kuharibu usalama haitakubalika na ikiwa kuna dukuduku Fulani ni muhimu kwa upinzani kwenda mahakamani kuliko kuandamana na kusabisha hali isio kuwa ya kawaida wakati kuna ugeniĀ .