DRC

DRC yapata spika mpya wa Bunge Vital Kamerhe

APRILI 24, 2024
Border
news image

Saa chache baada ya Bunge la Congo kupata Spika mpya wa Bunge ,wakaazi waomba kiongozi huyo kusadia wanainchi wa Congo kupata sheria mpya ambazo zina manufaa kwa wakaazi hasa Kuhsu usalama wa taifa ambalo laendelea kupitia shida za usalama hasa eneo lake la Mashariki ambako kuna uasi wa M23 wilayani Rutshuru,Masisi na sehemu moja ya Nyiragongo.Na eneo ;linginie kukiwa Kundi la kigaidi la ADF linalo wauwa raia kila siku kukicha .

Mumbere Bwana Pua mbunge wa Goma Kivu Kaskazini asema uchaguzi wa spika Mpya wa Congo DRC ni ishara tosha kuonesha kwamba udemokrasia unaendelea kushika kasi nchini ,kwani wagombea walikuwa watatu lakini wabunge waliamua kumchagua Vital Kamerhe kuwa kiongozi wao kwani lazima mikoa yote iwakilishwa katika serikali.

Wakaazi wa kwa upande wao wakiomba serikali kupunguza malipo ya wabunge na pesa nyingine kuwekwa katika usalama wa taifa hasa kwa wanajeshi wanao pigana kila siku kwa ajili ya usalama.pamoja na wenginekuomba Bunge lishughulikie haraka swala la usalama mashariki mwa Congo na kutafuta njia haraka kuwarejesha nyumbani wakimbizi wanao patikana kambini Mjini Goma.

Huku taifa likisubiri muundo wa serikali mpya kwa ajili ya mabadiliko ya utendaji kazi .wachambuzi wakiomba Rais wa Taifa kuchagua vijana na kufanya mabadiliko katika siasa kuliko kuweka watu wamoja kila siku katika uongozi ,Congo ikiwa ya Raia wote na kuepuka kuweka Taifa kuwa la Familia.

AM/MTV DRC ONLINE