Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Jamhuri ya Afrika ya Kati imeweka makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi kati yake na Africa ya Kati baada ya mawaziri wa ulinzi wa mataifa mawili kukutana mjini Kinshasa.
Mkataba huo wa ushirikiano wa kijeshi umetiwa saini Ijumaa hii, Oktoba 18, 2024, na Waheshimiwa GUY KABOMBO MWADIAMVITA @GuyKabombo na RAMEAUX-CLAUDE BIREAU, Naibu Waziri Mkuu wa Ulinzi wa DRC na Waziri wa Ulinzi na Ujenzi wa Afrika ya Kati.
Lengo ikiwa ni kuimarisha ushirikiano kati ya majeshi ya mataifa hayo mawili kwa lengo la kupambana vilivyo na changamoto za pamoja za kiusalama na kuendeleza amani na utulivu katika ya mataifa mawili.
Ushirikiano huu wa kijeshi kati ya Kinshasa na Bangui unaashiria enzi mpya ya ushirikiano wa kimkakati na mshikamano wa kikanda.