TANZANIA

DKT. BITEKO AONGOZA MAPOKEZI YA NAIBU WAZIRI MKUU WA CHINA

JANUARI 22, 2024
Border
news image

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati nchini Tanzania Mhe. Dkt. Doto Biteko leo ameongoza mapokezi ya Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Liu Guozhong ambaye yupo nchini kwa ziara ya Siku Tatu.

Akiwa nchini, Mhe. Guozhong anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.

Pia, atatembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na eneo la makaburi ya Wataalam wa kichina waliofariki wakati wa ujenzi wa reli ya TAZARA pamoja na Makumbusho ya Taifa.

Oliver G Nyeriga - MTV Tanzania