TANZANIA
Dk. Tulia Aongoza Kamati Ya Uongozi Dodoma
AGOSTI 28, 2023
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson ameongoza kikao cha kamati ya uongozi kilichopokea na kujadili Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano wa Kumi na Mbili (12) wa Bunge leo tarehe 28 Agosti, 2023 katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Mkutano huu wa wiki mbili utaanza kesho tarehe 29 Agosti, 2023 na unategemewa kuhitimishwa tarehe 8 Septemba, 2023.