TANZANIA

Dkt. Tulia Ackson Achangia Shilingi Milioni 24.7 Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Tanzania

SEPTEMBA 11, 2023
Border
news image

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson leo tarehe 11 Septemba, 2023 amekabidhi hundi yenye thamani ya shilingi mil. 24.7 kwaajili ya ununuzi wa tofali 9000 ili kusaidia ujenzi wa jengo la upasuaji wa Moyo na mishipa ya fahamu kama mchango wake wa ujenzi ikiwa ni sehemu ya ahadi aliyoitoa mnamo tarehe 9 agosti, 2023.

Akiongea wakati wa kukabidhi hundi hiyo, Dkt. Tulia Ackson ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya mjini, ameeleza kuwa kutokana na juhudi ambazo zimekuwa zikifaywa na Serikali pamoja na watendaji wa hospitali katika kuboresha huduma za afya imemuongezea hali ya kuendelea kutoa mchango wake kwaajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais. Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“..kwanza nitumie fulsa hii kuwapongeza sana kwa hatua mbalimbali mnazozichukua kuhakikisha huduma za afya zinakuwa bora zaidi katika hospitali yetu hii ya Kanda, mnafaya bidi ndio maana na sisi wengine tunawaunga mkono.” – Dkt. Tulia Ackson

Aidha, Dkt. Tulia Ackson ametoa rai kwa wadau wengine kuendelea kujitolea bila kujali kidogo walichonacho kwaajili ya kuhakikisha ujenzi wa jengo hilo unakamilika na hivyo huduma zinazotalajiwa zipatikane kwa wakati.

“..na pia ninawashukuru wadau ambao wameendelea kujitole kwa hivyo naamini wadau wengine wataendelewa kujitolea ili nao waje hapa wapite waone ni kitu gani kinahitajika na hata kama mchango wao ni mdogo utapokolewa.” - Dkt. Tulia Ackson

Nae, Dkt. Godlove Mbwanji Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, akipokea msaada huo amemshukuru Dkt. Tulia Ackson kwa moyo wake wa uzalendo kwa kuendelea kutekeleza ahadi zake za kimaendeleo ili kuwaletea maendelea zaidi na kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa Nyanda za Juu Kusini.

Dkt. Mbwanji ameeleza kuwa ujenzi wa jengo la upasuaji wa moyo na mishipa ya fahamu ni moja mikakati ya hospitali katika kuboresha huduma zake kwa jamii ndani na nje ya mipaka ya Tanzania katika kuunga fikra chanya za Mhe. Rais za nchi ya Tanzania kuwa kitovu cha Utalii wa Tiba Mbeya ikiwa ni lango kuu la nchi za SADEC.

“…Mbeya kimsingi katika mikoa mbalimbali kupitia hospitali zilizopo iko kimkakati katika mpango wa taifa wa kuongeza Utalii wa Tiba kuvutia wananchi kutoka nchi zinazotuzunguka kuja kupata matibabu.” – Dkt. Godlove Mbwanji

Dkt. Dino Mwaja ni mwenyekiti wa mradi huo amesema kwa sasa mradi huo upo katika hatua za awali hivyo ameshuru kwa mchango huo kwa kuwa utaenda kuongeza kasi na hivyo kupelekea mradi huo kuisha ndani ya muda uliopangwa.

“pia nikushukuru kwa mchango huu kwani utaenda kuongeza kasi ya ujenzi na tunaamini kwamba tutamaliza ndani ya muda uliopangwa.” - Dkt. Dino Mwaja.

Kukamilika kwa ujenzi huu wa jengo la upasuaji wa Moyo na mishipa ya fahamu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kutarahisisha upatikanaji wa huduma kwa urahis kwa wakazi wa Nyanda za Juu Kusini pamoja na wakazi wa nchi Jirani ikiwemo Zambia, Kongo, Msumbiji na Zimbabwe.

Oliver G Nyeriga - MTV Tanzania