TANZANIA

DK. BITEKO NA BASHUNGWA WASHIRIKI MISA YA KUMUOMBEA HAYATI MAGUFULI

MACHI 17, 2024
Border
news image

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati nchini Tanzania, Dkt. Doto Biteko na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa wameungana na familia na waumini kushiriki Misa Takatifu ya kumuombea Rais wa awamu ya Tano, Hayati Dkt. John P. Magufuli,leo tarehe 17 Machi 2024

Misa hiyo imefanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Yohana Maria Muzeyi wilayani Chato mkoa wa Geita na kuongozwa na Makamu Askofu, Padri Ovan Mwenge wa Katoke Seminari.

Misa hiyo Takatifu ya kumuombea Rais wa awamu ya Tano Dkt. John Magufuli inafanyika ikiwa imetimia miaka mitatu tangu alipofariki dunia Machi 17, 2021 ambapo imehuduliwa na familia ikiongozwa na Mke wa Hayati Dkt. Magufuli, Mama Janeth Magufuli, Watoto wa Hayati, Wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki.

MTV Tanzania