Gereza kakwangura ni mmoja wapo wa gereza ambazo zina wafungwa wanao pitia hali ngumu ya Kimaisha ikiwemo wanawake na Watoto ,gereza ambayo ilijengwa kwa ajili ya watu tano kwa sasa ikiwa na watu Zaidi ya thelani swala linalo wakera wanawake .
Kufatia hali hiyo Muungano wa mashirika ya akina mama kwa ajili ya kutetea haki za wanawake na Watoto SAFDF wakiungana na COLIBRI DRC, wamesaidia katika ujenzi wa chumba cha wanawake .Zawadi Visomeko ni katibu mtendaji wa SAFDF .
MOWA BAEKI-TELLY Roger akiwa mea Mji wa butemo amepongeza hatua ya akina mama kusaidia ujenzi wa chumba kimoja cha Gereza na kukumbuka hali wanayo pitia wanawake wanzio.
ZAWADI BISOMEKO, akiwa katibu mtendaji wa shirika la SAFDF akipongezahata hivyo serekali Kwaku wakubalia wanawake kujenga na kuboresha chumba kimoja cha gereza kwa ajili ya wanawake kwenye gereza ya Kakwangura Mjini Butembo Kivu Kaskazini
Utafahamu kwamba Grereza la kakwangura lilijengwa kwa ajili ya watu wachache lakini kwa sasa likiwa na watu Zaidi ya elfu moja wengi wao wakiwa wagonjwa na wengine wakiwa katika hali mbaya ya malisho .Mfano chumba cha wanawake kilijengwa kwa ajili ya watu wa tano lakini kwa sasa kuna wanawake ishirini na nane wengi wakilalamikia harufu mbaya Gerezani .
MTV ilifanikiwa kuzungumuza na mama mfungwa mmoja tukihifadhi jina lake asema mbali na kulala vibaya kuna watu wa usalama wanao watendea vitendo vya ngono wanawake nyakati za usiku waki wadanganya kuwa wata watetea ili waachiliwe .
wengine wakiwa gerezani bila hata kusikilizwa na kwa sasa wakiwa na Zaidi ya mwaka mmoja bila kufahamu hatma yao na bila kufahamu hukumu yao.Gereza nyingi kwa sasa zikishuhudia vitendo vya ubakaji wa wanawake lakini wakikaa kimia .
Muhindo wasivinywa wakili katika mji wa Butembo akisema tangu uongozi wa kijeshi mashariki mwa Congo hali ni mbaya na wafungwa wameongezeka wengi bila kusikikilizwa ma jaji wakiwa bila kusikiliza kesi za watu wanao fungwa gerezani na gereza kugeuka njia ya kifo kwa moja kwa sasa .
Katika mwaka mmoja wafungwa sabini wamefariki Dunia katika gereza ya kakwangura mjini Butembo hii ikiwa vile vile katika mikoa na miji mingine.
Utafahamu KWAMBA kagwangura ilishambuliwa na watu wanao dhaniwa kuwa ADF mwezi wa nane elfu mbili ishirini na mbili na wanawake kuishi Maisha magumu ndio sababu SAFDF Butembo imelazimika kujenga upya chumba chao na kuweka vitanda vizuri akisema Kambale Sivanzire Serge wa MTV akiwa katika Mji wa Butembo.