TANZANIA

AKATWA MAPANGA 19 AKIDAI HAKI

FEBRUARI 06, 2024
Border
news image

Bwana Geofrey Mboje Mkazi wa Katavi anusurika kifo nakuliomba Jeshi la Polisi nchini kuwasaka nakuwachukulia hatua watu 6 waliomkata mapanga 19 mwilini wakati wakimzuia asidai haki zake na wananchi wenzie ya kumiliki ardhi huku akiomba msaada kwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuwasaidia wapate haki yakumiliki eneo la hekali 3500.

Ameomba msaada huo mbele ya wananchi wa Kijiji cha Nsimbo ambapo walizuia msafara wa Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Paul Makonda nakumueleza mbali na kukatwa mapanga bado wanatishiwa maisha na watu hao na familia zao zipo hatarini.

Alisema ugomvi huo uliwahi kusuluhishwa na Mkuu wa Wilaya ambapo aliamuru eneo hilo lirudishwe kwa wananchi hao na ndipo vikaanza visa vya kutishiwa na kukatwa mapanga 19 mwili mwake hali iliyompelekea kulazwa siku 30 Hospital kwa kutumia gharama zake mwenyewe.

Katika kumsaidia mtu huyo ajikimu kimaisha Mwenezi Makonda alimpa posho yake ya siku ikamsaidie kuendesha maisha yake wakati akisubiria vyombo vya dola kuchukua hatua za haraka nakuongeza kuwa Rais wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan hatafurahi kusikia wananchi wake wanateswa nakuonewa kwani amekua ni kinara wakusimamia haki za watu wote bila ubaguzi nakuwauliza polisi ni lini watawalinda wananchi?

MTV Tanzania