TANZANIA

Ajira Zaidi Ya Elfu 20 Kutolewa Tamisemi Tanzania

SEPTEMBA 17, 2023
Border
news image

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa nchini Tanzania Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Ofisi yake imapata kibali na katika kipindi cha mwaka huu wa Fedha itatangaza ajira zaidi ya elf ishirini kwenye Kada ya Ualimu na Afya.

Waziri Mchengerwa ameyasema hayo Wilayani Newala wakati alitoa salamu za Wizara yake kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Wilayani hapo.

Amesema Mhe. Rais kupitia Ofisi yangu tuliomba Kibali cha ajira kupitia Ofisi ya Rais - Utumishi na wewe mwenyewe ukaridhia kuwa katika mwaka huu wa fedha tuajiri watumishi 20,600 ambao wana upungufu zaidi kwenye Halmashauri.

‘Kila Halmashauri tunayopita ombi kubwa limekua ni Watumishi wa Elimu na Afya na kukujali hiyo ulishatupa Kibali cha kuajiri hivyo wakati wowote ndani ya mwaka huu wa Fedha tutatangaza Ajira hizo na tutaleta watumishi kwenye Halmashauro hii ya Newala’ alisema Mchengerwa.

Kupitia Ajira hizi Halmashauri zote zitapata watumishi kwenye maeneo hayo na kwa hapa Newala tutawapatia watumishi 130 wa Kada za Elimu na Afya’ alisisitiza.

Akizungumzia Wilaya ya Newama amesema Serikali kupitia TARURA itaongeza mtandao wa barabara ya Lami yenye urefu wa Km 6 ambapo Newala Mji watapata Km 3 na vijijini watapata km 2.85; Aidha Taa za barabarani zitaongezwa Taa 48 ambazo zitasaidia kupendeza mji na kuongeza ulinzi.

Kama tunavyofahamu kuwa hii ni Wilaya Kongwe na hata hospitali ya Wilaya iliyopo ina uchakavu mkubwa hivyo tumeleta Shilingi Million 900 lwa ajili ya kufanya ukarabati wa hospitali hiyo kongwe’ alisema Mje. Mchengerwa.

Mhe. Rais Skt. Samia Suluhu Hassan yupo Mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi na meo ametemebelea Halmashauri ya Mtwara Dc, Nanyamba Mji, Tandahimba, Newala na Masasi.

Oliver G Nyeriga - MTV Tanzania