DRC

Abiria Zaidi Ya Kumi Waokolewa Katika Ajali Mpya Ya Meli Kwenye Ziwa Kivu Mashariki Mwa Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Congo

OKTOBA 28, 2024
Border
news image

Kwa mjibu ya vyanzo vyetu vina thibitisha ajali hio ikiwa ni pamoja na serikali ya mkoa wa Kivu Kusini mashariki mwa Congo,vyaonyesha kuwa ni mtumbwi moja uliokuwa ukitoka katika mji mdogo wa MINOVA kuelekea mji wa BUKAVU mji mkuu wa mkoa wa KIVU KUSINI ambao ulipinduka karibu na KASANYU, kijiji kilichoko katika wilaya la KALEHE jumapili oktoba 27,2024.

Vyanzo vyetu vya dai kwamba ajali hii ya meli ilitokana na hali mbaya ya hewa katika ziwa hilo ambayo iliambatana na mvua kubwa.

Matokeo ni kwamba karibu watu kumi waliokuwa ndani ya meli hiyo waliweza kuokolewa, vyanzo hivi vikithibitisha kuwa hakuna kifo kilichoripotiwa tofauti na mtumbwi huo pamoja na baadhi ya watu, bidhaa ambavyo vilipinduka.

Kuzama kwa meli hio kunakuja karibu mwezi mmoja baada ya kuzama kwa mashua MERDI mnamo Oktoba 3,2024 ajali ya meli iliyobeba mamia ya watu, kulingana na vyanzo duru zetu zikithibitishwa na duru za serekali ya DRC Licha ya hatua zilizochukuliwa na mamlaka kuzuia aina hii ya ajal, wamiliki wa meli bado hawajaweza kuheshimu.

wanaharakati kadhaa wa mashirika ya kiraia na watetezi wa haki za binadamu, waendelea ku laumu visa vya ajali za meli katika ziwa KIVU na ziwa nyingine nchini.

AM/MTV News DRC