DRC ITURI

UCHUNGUZI WAHITAJIKA BAADA YA RAIA WA CHINE KUSHAMBULIWA NA WATU WENYE SILAHA LWEMBA WILAYANI MAMBASA.

Aprili 03, 2024
Border
news image

Watu wa wili wafariki Dunia na wengine kujeruhiwa wakati wa shambulizi la watu wenye silaha wanao dhaniwa kuwa nikutoka mai mai,miongoni mwa walio fariki Dunia Raia mmoja wa chine na nmkaazi wa mahali.

Shambulio hili lilitokea Mambasa kilometa 160 kusini na mji wa Bunia Mkoni Ituri katika kijiji mahulo barabara ya Kisangani . Mlio wa risasi ulisikika hii tarehe mbili kwenye misitu eneo la uchimbaji madini la Malutu katika eneo Teturi usultani wa Babila Babombi.

Duru zetu za mahali za sema kwamba raia wa chine walipigwa risasi wakati walikuwa wakiondoka eneo la uchimbaji madini la Malutu ambako raia hao wamesha piga kambi kwa muda mrefu wakichimba halmasi na madini mwengine.Raia wa chine wengi huwawa mkoani Ituri na kushutumiwa katika uchimbaji wa kimagendo kwa muda mrefu katika eneo nyingi za Congo .

Mashirika ya ki raia ikiomba uchunguzi kufanyika kwa haraka na kuwakamata wahusika wa shambulizi hilo. Utafahamu kwamba siku zilizo pita raia wengine wa chine walishambuliwa na kuwawa kwa risasi katika tukio kama hilohilo Mkoni Ituri .

Wakaazi wa eneo hilo wasema madi yao imekuwa ikichimbwa bila wakaazi kufaidika hii yaweza kuwa sababu ya kuweko mzozo kati ya raia wa chine na wakaazi wa mahali.Migodi nyingi ya Ituri hulindwa na jeshi tiifu kwa serikali hata askari polisi .lakini wakishambuliwa na watu wenye silaha.

Wakaazi tulio zungumuza nao wasema mali yao imekuwa ikiporwa na watu kutoka mataifa ya kigeni na shamba zao kuharibiwa na baadae kubaki fukara bila mafanikio yoyote na miradi ya maendeleo.

Nadège Mulemba.