DRC GOMA UJENZI WA SOKO YA KAHEMBE

SERIKALI KATIKA USHIRIKIANO NA KAMBUNI INOV waweka mikakati ya maandalizi ya ujenzi wa Soko Kubwa ya Kahembe Katika Mji wa Goma Kivu Kaskazini.

JANUARI 30, 2024
Border
news image

Akizungumuza na MTV DRC ONLINE baada ya kukutana na Gavana waw a Kijeshi PETER CIRIMWAMI ,PASCAL MOISE mkuu wa kambuni ya INOV asema kambuni yao kwa sasa imejipanga kushirikiana na serikali katika ujenzi wa soko Muhimu ya Kahembe katika eneo la Birere ikiwa karibu na Mpaka wa DRC na Rwanda.

PASCAL MOISE mkuu wa kambuni ya INOV anasema mradi huo kwanza utawapa ajira vijana,kupunguza msongamano wa ma gari kwenye BARABRA kuu inayo kwenda uwanja wa Ndege wa Goma na kuwaondoa wafanya biashara wanao baki barabarani kuuza vyakula vyao na kusababisha ajali nyingi za mara kwa mara.

Baada ya kukutana na Gavana wa Kivu Kaskazini watendaji wa INOV wasema hivi karibuni wataanzisha ujenzi kwa haraka na kwa kasi kubwa Mradi muhimu wa Maendeleo kwa ajili ya Mji wa Goma .na ujenzi huo utasidia serikali kupata mapato kutoka Kodi 

AM/MTV