TANZANIA

RAIS DK.MWINYI ASHUKURU KWA DUA ZA HAYATI MZEE MWINYI

Aprili 10, 2024
Border
news image

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema familia ya Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi imefarijika sana tangu alipofariki dunia kwa Dua zilizofanyika katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kumuombea.

Ameshukuru kwa Dua zilizosomwa kumuombea Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo katika kisomo cha Dua ya Arubaini ya Hayati Ali Hassan Mwinyi pamoja iftari iliyofanyika viwanja vya Ikulu Mnazi Mmoja.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amesema ni siku ya kipekee asubuhi imefanyika Hitma ya kuombea Hayati Sheikh Abeid Amani Karume na jioni Hayati Ali Hassan Mwinyi.

Dua hiyo imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyombo vya ulinzi na usalama, Dini , Vyama vya Siasa na Wananchi.

MTV Tanzania