DRC BENI

MASHIRIKA YA KIRAIA YA KIRAIA KATIKA MJI WA BENI NA WILAYANI YAOMBA SERIKALI KUZIDISHA USALAMA WA WANANCHI .

Aprili 05, 2024
Border
news image

Mashirika ya kiraia katika mji wa Beni kivu Kaskazini yaomba jeshi kuongeza juhudi zake baada ya shambulizi la ADF huko Magodomu.

Akizungu na vyombo vya Habari Vya mahali siku chache baada ya watu wenye silaha kushambulia kata la MANGODOMU kata moja ya Mji wa Mangina kilometa Zaidi ya ishrini magharibi mwa Mji wa Beni .PEPE KAVOTA mwanaharakati wa kutetea haki za binaadamu aomba serikali yake Felix Tshisekedi kubalisha mbinu zake za kupambana na waasi wa ADF wanao kuwa katika misitu ya Beni wanao kuja kuwashambulia wakaazi wasio kuwa na hatia.

Kavota aliongeza kuwa juhudi zinahitajika kwakuwalinda wananchi wa Beni na wilaya zake ambao kumeshuhudiwa mauaji ya mara kwa mara kwa Zaidi ya miaka kumi hadi sasa .wakaazi wakilazimika kuhama makaazi yao na kukimbilia miji yenye usalama kama Butembo,Beni Mjini.Bunia,Kisangani ,Goma na wengine hata katika mataifa Jirani. . .

Mratibu wa shirika la raia Mjini Beni aomba serikali kuzingatia swala la usalama wa wakaazi kwani sasa kwa sasa mashambulizi imedhidi kiasi kwamba wakaazi wameonekana kuchoshwa na hali hii ya ukosefu wa usalama ilio anza tangu mwaka wa elfu na kumi .Mauaji ya hivi karibuni lilitokea juma nne katika kata la Mangodomu ambako vyombo vya usalama vilishutumu wapiganaji kutoa kundi la ADF ambako watu Zaidi ya kumi waliuwawa kwa kupigwa risasi na wengine kwa mapanga .

Utafahamu kwamba kwa sasa serikali ya Congo inashirikiana na jeshi la wananchi wa Uganda UPDF katika msako wa ADF lakini ADF bado ikiendelea na harakati zake.

ADF ilipata nguvu Zaidi baada ya kushambulia gereza ya Butembo ambako iliwabeba wafungwa Zaidi ya mia nane (800) na gereza nyingine katika mji wa Beni Kivu kaskazini ambako wafungwa Zaidi y amia saba nao walitekwa na waasi hao na kuongeza idaidi ya wapiganaji wa ADF.

Kwasasa wakaazi washutumu serikali kushindwa kulinda raia zidi ya mashambulizi ya ADF na kuwalazimisha kuhama makaazi na vijiji vyao . Mbali na jeshi la Uganda Beni kuna kikosi kikubwa cha MONUSCO yaani Umoja wa Mataifa ambao hutazama namna wananchi wanavyo uwawa na vijiji vyao kuchomwa moto. Japo majuku yao DRC nikulinda raia dhidi ya maafa ,jukumu ambako UN imeshindwa kutekeleza yasema mashirika ya kiraia.Kivu Kaskazini na Ituri.

Nadège Mulemba. MTV DRC ONLINE