DRC Wazalendo

Makundi ya wazalendo mashariki mwa Congo yatangaza kuendelea kulinda usalama na vijiji vyao dhidi ya uvaamizi japo baadhi ya wapiganaji wake waendelea kupoteza Maisha kwenye uwanjwa wa Mapigano.

Machi 26, 2024
Border
news image

Akizungumuza na MTV DRC ONLINE Mmoja wa makamanda wa Kundi la wazendo kutoa nyiragongo asema wenzao kufariki kwenye uwanja wa Mapigano haiwezi wateteresha bali wakuapa juhudi Zaidi

Kamanda Mbokani mkuu wakikundi cha UFDPC na apongeza wakaazi wa Mji wa Goma Na nyiragongo na juhudi zao za kuwaunga mkono wakati wowote na wakati mgumu ambao wamepitia wakupoteza mmoja wa Kamanda wao wakati wa mapigano katika Mji wa Kibumba juma mosi.

Wazalendo ni makundi ya vijana kutoka makabila mbali mbali na sehemu mbali mbali wanao kabiliana na Uasi wa M23 wilayani Masisi na nyiragongo kwa Zaidi ya mwaka mmoja sasa ,wengi wakiungwa mkono na wananchi wa Congo katika kile wanacho kiita uvaamizi.Vijana wengi mashariki mwa Congo hasa Masisi,Nyiragongo ,Rutshuru na Lubero wako kwenye mustari wa mbele wa mapigano wakiunga mkono juhudi za jeshi katika Mapigano yaitwa ya uvaamizi kutoka ma Taifa Jirani ya Congo .

Wazalendo wasema wenzao walifariki Dunia wakati wa mapigano makali siku ya juma mosi katika Mji wa Kibumba unao patikana kwenye kilometa ishrini Kaskazini mwa Mji wa Goma na hii itawapa juhudi Zaidi kwakupiginia ardhi yao asema Kamanda Mbokani .

AM/MTV DRC ONLINE