TANZANIA

Gavana Wa Kivu kaskazini meja jenerali PETER CIRIMWAMI atishia kuwakamata na kuwachukulia hatua kali mahakamani watu wote wanao husika katika ukosefu wa usalama Mjini Goma hasa wanajeshi,wazalendo ..

Aprili 12, 2024
Border
news image

Akiwa na hathira kubwa kutokana na ukosefu wa uslama unao tekelezwa na watu wenye silaha Mjini Goma Piter Cirimwami aonya mutu yeyeto atakae patikana katika maswala ya ujambazi ama uhalifu wowote atakamatwa na kufikishwa mahakamani

Katika wiki moja watu Zaidi ya kumi wameuwawa mjini Goma na watu wenye silaha ambao wakaazi washutumu kutoka jeshi tiifu kwa serikali na wapiganaji kutoka Vijana Wazalendo .wengi wanao uwawa wakipigwa risasi hatua hii imechukuliwa kufatia visa kadhaa ambavto vimeripotiwa Mjini Goma hasa vya mauaji,wakaazi katika Mji wa Goma kwa sasa wakiishi katika sinto fahamu na tumaini ya kuishi ikiwa tatizo.

Katika kikao Cha usalama kilicho fanyika hii alhamisi kunako ofisi ya gvana hatua kali zimechukuliwa ,ikiwemo kupiga marufuku watu kutembea na silaha Mjini Bila sababu,kila kamanda wa kikosi cha wazalendo kuweka discipline kwenye wapiganaji wake,kila kamanda wa jeshi kuzuia wanajeshi wake kuzurura mitaani bila sababu wakiwa na silaha.

Kamanda wowote atakae kiuka amri atakamatwa na kufikishwa mahakamani.Watu wanao miliki silaha wamekuwa waki wauwa watu na ku pora mali ya wakaazi kwa nyakati za jioni ama mchana kutwa bila kutishwa ,serikali ikiombwa kuhakikisha uaslama wa wakaazi unapatikana kwa haraka.Mji wa Goma kwa sasa unapitia hali mbaya ya usalama kila mkaazi akiishi katika uhoga Mkubwa ,watu wakikutwa wameuwawa na watu wasio julina. Pamoja na watu wanao dhaniwa kuwa polisi kuwanyanganya simu wakaazi saa za usiku wanapo fanya doria.

Nadège Mulemba.