DRC

Gavana wa Kivu Kaskazini Meja Generali PETER CIRIMWAMI Aaapa kuendelea na ujenzi Pamoja na miradi ya maendeleo katika Mkoa wake

MACHI 19, 2024
Border
news image

Akizungumuza na MTV DRC ONLINE Meja Generali PETER CIRIMWAMI alisema pesa za wananchi wa Congo lazima kusaidia wakaazi husika ndio sababu ameamua kurejesha pesa za Kodi zao katika Miradi ya maendeleo ya miji yao Pamoja na kuwapa ajira Vijana kwanza Pamoja na Kambuni za Congo zenyewe kufaidika kwa ujenzi wa taifa lao

Cirimwami alisema hayo mwishoni mwa wiki juma mosi baada ya kufanya mzunguuko mjini na kamati ya usalama wa Mkoa ambako walitemebea miradi ilio pewa kwa kambuni mbali mbali Vijana wakipongeza hatua za PETER CIRIMWAMI kama felicien Tumsifu mmoja waw a Vijana maaruhu Mjini Goma .Tumsifu anasema hatua ya Gavana wa Kivu Kaskazini ni ya kuunga mkono kwani inafanyika wakati mkoa uko kwenye matatizo ,ingekuwa kuna usalama angefanya hatua Zaidi.

Huku waendeshaji pikipiki nao wakiwa wa kwanza kupongeza kazi zake PETRE CIRIMWAMI Gavana kwa muda wa Mkoa huu.Mkoa wa Kivu Kaskzini una shuhudia mapigano ya hap ana pale hasa uasi wa M23 lakini gavana alisema hii haiwezi kuzuia miradi ya maendeleo.Utafahamu kwamba miradi kadhaa ya maendeleo imeanzishwa katika mji wa Butembo ,Beni na Goma ikiwa ni hatua kubwa katika utawala wa Kijeshi Kivu Kaskazini.

AM/MTV DRC ONLINE